Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van Gaal, ambaye kikosi chake kina tatizo la safu ya ulinzi. Agosti 30 Sportsmail ilieleza kuwa suala lililokuwa limekwamisha kibali chake cha kazi ni kwamba maafisa wa ubalozi walikuwa wakichunguza taarifa za tuhuma ya malumbano kati ya Rojo na jirani yake nchini Argentina.
Muargentina huyo, hakuwahi kushtakiwa kwa tukio hilo, ambalo lilitokea mwaka 2010, ila bado lilikuwa likifanyiwa uchunguzi wa kinadharia baada ya kesi kufunguliwa upya mwezi Mei mwaka huu
Post a Comment