0

Mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid Cristiano Ronaldo ameupongeza uongozi wa klabu ya Man Utd kwa kufanikisha mipango ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Colombia Radamel Falcao akitokea AS Monaco kwa mkopo wa muda mrefu.
Ronaldo ambaye kwa sasa amejiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya michezo ya kimatafa itakayochezwa mwishoni mwa juma hili amesema kusajiliwa na Falcao huko Old Trafford kutaibua hisia mpya za ushindi.
Amesema Falcao ni mshambuliaji mwenye sifa za kipekee na mwenye uwezo wa kuisaidia klabu yoyote pale inapomuhitaji hivyo anaamini matatizo yaliyoikabili Man Utd tangu mwanzoni mwa msimu huu yatakwisha.
“Ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa hivyo kwenda kwake Man Utd kutakuwa na hisia tofauti kwa wachezaji wengine ambao walionyesha wana jambo ama kitu wanakihitaji kwa lengo la kufikia malengo ya ushindi.” Amesema Ronaldo
Hata hivyo Ronaldo ametoa tahadhari kwa mashabiki wa Man Utd kutotarajia mambo mazuri kwa haraka kutoka kwa Falacao zaidi ya kumpa muda wa kucheza michezo miwili hadi mitatu na ndipo wataanza kuona mabadiliko ya kushangilia ushindi.

Post a Comment

 
Top