tetemeko la ardhi nchini China
Wafanyakazi wa uokoaji nchini
China wanaendelea kujitahidi kufikia eneo la lilipigwa na tetemeko la
ardhi katika jimbo la Yunnan siku ya jumapili na kuua watu zaidi ya mia
tatu na themanini.
Kikosi cha dharura kinajaribu kukarabati
barabara zilizoharibiwa ili kuwezesha usafiri katika maeneo yaliyopata
mvua kubwa na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.Maelfu ya watu waliodhurika na tetemeko hilo wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa na mamlaka zinazohusika.
Shuhuda mmoja amesema karibu theluthi mbili ya nyumba zimeharibiwa katika kijiji chao.
Maelfu ya mahema na vitanda vya dharura vimepelekwa katika eneo hilo liloathirika na maelfu ya wafanyakazi wa idara ya dharura watumwa kusaidia kazi ya uokoaji.
Post a Comment