Kobe huyu anasemekana alitoroka kwa hofu ya kukamatwa na polisi
Polisi mjini Los Angeles
Marekani wamefanikiwa kumshika tena Kobe mkubwa aliyetoroka baada ya
kinachoelezewa kama harakati ndogo za kumkimbiza Kobe huyo katika
barabara za mji huo.
"Kobe huyo alijaribu kukimbia lakini maafisa
wetu walikua na mbio zaidi," ilinukuu taarifa ya idara ya polisi ya
Alhambra kwenye ukurasa wake wa Facebook.Maafisa wawili wa polisi walifanikiwa kumbeba mnyama huyo na kumuweka ndani ya gari la polisi.
Kobe huyo kwa jina Clark alipelekwa katika kituo cha wanyama waliookolewa ambapo hatimaye alijiunga na wamiliki wake.
Kumfuga mnyama huyo bila ya idhini ya maafisa wakuu ni kinyume na sheria, lakini polisi hawatawafungulia mashitaka wamiliki wake.
Kobe wana uwezo wa kukimbia kasi ya kilomita 1.6 kwa saa ikiwa wanataka.
Post a Comment