Mamia ya watu nchini Ukraine bado wanakumbwa na hali ngumu ya kibinadamu
Urusi inasema kuwa karibu malori
300 yaliyosheheni misaada ya kibinadamu yameondoka mjini Moscow
kuelekea mashariki mwa Ukrain kufuatia makubaliano na Ukrain ya kuwepo
msaada wa dharura chini ya uongozi wa shirika la kimataifa la msalaba
mwekundu.
Vyombo vya habari nchini Urusi vinasema kuwa
msaada huo utapokelewa kwenye mpaka na Ukrain na shirika la kimataifa la
msalaba mwekundu na kupelekwa kwa raia waliojipata kwenye mapigano
mashariki mwa Ukraine.Lakini shirika la Red Cross linasema kuwamaelezo kuhusu mpango hauo bado hayajatolewa.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesema kwamba lazima ihahakikishwe kwamba hatua hiyo ya Urusi sio njamaya Urusi kutaka kuingilia hali katika eneo hilo.
Post a Comment