Kampuni kadhaa za Marekani,
zimeahidi kuekeza dola bilioni 14 barani Afrika hasa katika sekta ya
kawi na miundo msingi. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Rais wa Marekani
Barack Obama.
Tangazo hilo limetolewa katika mkutano wa kwanza
wa viongozi wa Afrika nchini Marekani. Mkutano wenyewe umehudhuriwa na
zaidi ya marais 40 wa bara hilo.Mkutano huu unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika huku China ikiendelea kuongeza uekezaji wake barani Afrika.
Rais Obama pia aliandaa maankuli ya jioni kwa niaba ya marais hao katika ikulu ya White house.
Mikataba hiyo iliyotangazwa Jumanne, ilijumuisha ushirikiano wa dola bilioni 5 kati ya kampuni ya Blackstone na Aliko Dangote, mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika kwa kuinua miradi ya kawi na miundo mbinu kuisni mwa jangwa la Sahara pamoja na uekezaji zaidi katika miradi ya kawi inayofadhiliwa na Rais Obama.
'Ustawi na maendeleo''
Benki ya dunia, ilitangaza kuwa itawekeza dola bilioni 5 katika miradi ya kawi huku kampuni ya General Electric ikisema imejitolea kuekeza dola bilioni 2 kusaidia miradi ya miundo msingi pamoja na kupiga jeki ustawishaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa kawi.
Rais Obama pia alisema kuwa Marekani itatoa dola bilioni saba za ziada ili kufadhili mradi wa kufanya biashara Afrika , na kufikisha ufadhili wa miradi ya maeneleo barani Afria hadi dola bilioni 33.
Post a Comment