Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo anayefanya kazi nchini Marekani amekabidhi mabegi 650, kila begi lina vifaa mbalimbali vya shule. Vifaa vilivyokabidhiwa na Flaviana Matata mwenyewe kwa baadhi ya wanafunzi wa wilaya za Nachingwea na Lindi Mjini
Lengo la msaada huo ambao umetolewa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Flaviana Matata na PSPF ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi nchini Tanzania anapata elimu akiwa na vifaa muhimu vinavyohitajika.
Hii ni mara ya pili kwa PSPF kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata kutoa msaada huo kwa wanafunzi, mwaka jana wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani Pwani walifaidika na msaada huo.
Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukijihusisha katika kusaidia maeneo mbalimbali yanayohitaji msaada ambao utaleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Tanzania.
Post a Comment