Mbaki ya ndege ya Algeria ilioaguka
Rais wa Ufaransa Franswa Hollande ameahidi kwamba mabaki ya raia 118 na wafanyikazi walioabiri ndege moja ya Algeria ilioanguka Magharibi mwa Afrika yatapelekwa nchini Ufaransa.
Rais Hollande ambaye alifanya mkutano na familia za waathiriwa wa Ufaransa ,amesema kuwa bendera zitapepea nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali kwa siu tatu mfululizo kuanzia jumatatu.
Amesisitiza umuhimu wa wa kubaini chanzo cha ajali hiyo iliotoea nchini Mali.
Awali wachunguzi wa umoja wa mataifa katika eneo la mkasa wanasema kuwa wamekipata kisanduku cha pili kinachorekod yanayojiriu katika ndege.
Post a Comment