0

Vifo zaidi ya 600 vimetokana na Ebola huko Afrika Magharibi.

Shirika la Afya Duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na mkurupuko wa maradhi ya Ebola katika maeneo ya Afrika magharibi, sasa imepanda na kufikia zaidi ya watu 600.
Yamkini watu wengine 68 wamefariki katika kipindi cha juma moja lililopita.
Maofisa wa matibabu wa kimataifa na wale wa maeneo hayo wanajaribu kuyafikia maeneo ya mataifa yaliyothirika na ugonjwa huo kama vile Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Changamoto zachelesha udhibiti wa Ebola Afrika Magharibi
Uvumi, wasiwasi,imani potovu na kutoaminiana kunachochea kusambaa kwa ugonjwa huo huku baadhi ya wanaviji huenda wangali wanawaficha wagonjwa wao kwa hofu ya kutengwa.
Ebola ni ugonjwa hatari unaosambaa kwa kasi mno hivyo huenda idadi kamili ya vifo vinavyotokana na Ebola isijulikane.
Baadhi ya waliowahi matibabu sahihi mapema wamepona.

Post a Comment

 
Top