Dar es Salaam. Bodi ya Taifa ya Uhasibu
(NBAA) imebadili mitalaa itakayotumika kuwatahini watahiniwa katika
daraja juu la uhasibu Certified Public Accountant (CPA) kwa lengo la
kuongeza ufanisi katika taaluma hiyo.
Mabadiliko hayo ya kimfumo yameenda sambamba na
upunguzwaji wa masomo ili kwenda sambamba na mabadiliko ya mazingira,
biashara na mwenendo ya ajira.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBBA, Pius Maneno alisema
tofauti na ilivyokuwa awali mitaala hiyo mipya imeundwa kwa mfumo wa
kuweza kutafsiri mafunzo kwa vitendo.
Alisema mfumo huo umelenga kumwelimisha mwanafunzi
ili aweze kutumia mafunzo na kuimarisha ubora katika utendaji wa kazi
ya uhasibu.
“Mitaala hii imekuja na mfumo tofauti kabisa na
uliokuwa hapo awali, ambao ulikuwa umejikita zaidi kwenye usomaji wa
nadharia ambao wengi walikuwa wanasoma kwa ajili ya kujibu mitihani,
sasa mwanafunzi anapaswa kuwa na uelewa wa hali ya juu na kutafsiri
mafunzo kwa vitendo,” alisema Maneno.
Mmoja wa wanafunzi waliojisalili kufanya mitihani
hiyo Novemba mwaka huu Julius Nyirenda alisema mabadiliko hayo yanaleta
unafuu kwa wanafunzi na kutoa hamasa ya wengi kufanya mitihani hiyo.
“Ni mfumo utakaowahamasisha wanafunzi wengi,”alisema.
Post a Comment