Dar es Salaam. “Naombeni msaada…Wananipiga
jamani…Tafadhari ndugu zangu niokoeni wataniuwa mimi,”…Ni sauti ya
kijana anayepigwa na kundi la vijana kutokana na tuhuma za wizi eneo la
Buguruni majira ya saa moja na nusu usiku.
Vijana hao wanaonekana wenye hasira kali na jazba
bila ya kujali malalamiko ya mwenzao wanaendeleza kipigo. Wakati kijana
huyo anaendelea kupokea kipigo kutoka kwa vijana hao walioukuwa
wanamvuta pembeni mwa barabara sambamba na kumchania shati lake, vijana
wengine watatu wanajitokeza na kuungana nao kuendeleza kipigo.
Ni jambo la kushangaza, hata wakati tukio hilo
linaendelea hakuna mpita njia mwingine aliyeonyesha kuguswa zaidi ya
vijana hao watatu.
Pilikapilika za watu katika eneo hilo zinaendelea
kama kawaida.Wengi wakiwa wanarejea katika shughuli zao mbalimbali za
kujitafuatia riziki za kila siku na wengine wanaendelea na biashara.
Kumbe katika harakati hizo za wengine kurejea
nyumbani baada ya kazi za siku, kuna wengine kwao ndiyo muda wa kutafuta
riziki.Kutafuta riziki huko kupo kwa namna tofauti tofauti. Kuna wale
wanatafuta kwa njia za hali na zile zisizo za halali ilihali tu mwisho
wa siku mkono uende kinywani bila ya kutiwa mikononi wa polisi wala
wananachi wenye hasira kali.
Tukizungumzia wale wanaotafuta riziki kwa njia
zisizo za alali tunamaansha watu wanaojihusha na wizi, uporaji, utapeli,
uporaji na kujiuza kwa maana ya kahaba.
Ujanja wa waporaji wa Buguruni
Wizi hasa wa mifukoni na kwenye mikoba hasa kwa
kinamama umezoeleka sana katika maeneo mengi yenye msongamano wa watu.
Ukizungumzia kwa wanawake juu ya suala hili basi kila mmoja anaweza
kukupa stori yake lakini kwa Buguruni hali ni tofauti.
Wezi wa eneo hilo hutumia mbinu tofauti ambazo
hazijazoeleka sana na vibaka wengine. Ukiwa mgeni wa eneo hili na kama
hufahamu vizuri jiografia ya hapo basi unaweza kuibiwa bila la
kujitambua.
Kutokana na hali ya watu kuwa wengi na
pilikapilika nyingine vibaka hutumia mwanya huo kutimiza malengo yao
japo kwa upande wao ni kujipatia riziki, lakini kwa njia isiyo halali.
Kwa muda wa kama saa takriban mbili mwandishi wa
gazeti hilo alipokuwa katika eneo hilo akishuhudia baadhi ya vijana
ambao huwa wanadaiwa kutembea kwa makundi nakujifanya kuwa wanagombana,
lakini ugomvi huwa machoni mwa watu wengine na wao wakiwa wamepanga
njama ya kuiba.
Siku hiyo kama bahati kwa gazeti hili,
lilishuhudia wakiwa kwenye harakati za kufanya tukio la wizi, kwani kwa
wazoefu wa eneo hilo wanasema vijana hao hutumia mbinu hiyo mara chache
ili watu wasiizoe.
Kundi hilo la vijana wapatao kumi hivi walitokea upande wa
Barabara ya Mandela kuanzia Buguruni hadi Tazara, wakiwa wanazozana na
kutupiana ngumi wengine wakiwa wanajifanya kama wanajaribu kuamua
ugomvi. Wakaendelea kuvutana hadi Tazara kuelekea kwenye kituo cha
daladala eneo hilo.
Mzunguko wa aina hiyo hufanywa kwa pande zote nne
kwa maana ya upande wa kituo cha daladala cha kuelekea Tazara, Ubungo na
Posta.
Kwa wazoefu wa eneo hili hasa wafanyabiashara
ndogondogo wanauza bidhaa mbalimbali tabia hiyo sito ngeni kwao. Hivyo
wao walionekana kutojali na kuendelea na shughuli zao, kuhudumia wateja
wao bila kutilia maanani ya kilie kilichokuwa kinajiri kwa wakati ule.
Pia kwa wapitanjia na watu ambao siyo wazoefu wa
eneo hili walibaki wameduwaa, wengine wakitamani kuingilia kati kuamua
ugomvi wa vijana hao waliokuwa wanapigana.
Katika kutaka kudadisi ili kujua hasa ni nini
kilikuwa kinaendelea, alidokezwa kuwa ugomvi ule ni mbinu ya vijana hao
kutaka kuiba na kupora vitu vya watu.
Wakati wanavutana vile na kutupiana ngumi ndani ya
lile kundi unakuta wameshamwibia mtu, sasa ili kuondoa wasiwasi kwa
watu wanafanya hilo ili wasitambulike na wakifika kituoni tena kwa wale
watakaokuwa wanashangaa, pia watakacho kutananacho ni halali yao.
Mathalan, jambo la kushangaza za zaidi ni kwa
jinsi vijana hao wasivyo na tone la huruma kwa wale wasamaria wema
wasiojuwa mbinu hiyo, ambapo wakijaribu kuamua ugomvi huo hujumuishwa
kwenye kundi hilo na kugeuzwa mwizi na kumpora kila kitu alichokuwa
nacho.
Pia, gazeti hili lilishuhudia abiria walioukuwa
wanasubiri daladala kituoni hapo wakinyakuliwa baadhi ya vitu vyao na
vibaka ambao wanajificha kwa miamvuli ya wapigadebe.
Kwa upande wa wizi huu hawa jamaa wanakuwa na utu
kidogo. Japo kwa abiria ambao ni wazoefu huwa wanajihami hasa
wanawake.Kinamama wengi wanapokuwa katika eneo hili hujitahidi kushika
mikoba yao kwa umakini wa hali ya juu.
Wale wanaobeba mabegi ya mgongoni kwa ajili ya
kompyuta mpakato (laptop), huwa wanageuza ubebaji wake na kuyabeba mbele
kwa maana ya kifuani badala ya mgongoni ili kuhakikisha usalama wa mali
zao.
Licha ya jitihada zote hizo za kujihami
wanazofanya abiria, bado hawa jamaa wamekuwa wakifanikiwa kupora watu
mali zao zikiwamo simu za mkononi na fedha.
Gazeti hili lilishuhudia jinsi ambavyo jamaa mmoja
alinusurika kupoteza vitambulisho vyake baada ya kibaka mmoja kumwibia
baada ya kwenda pembeni na kugundua siyo hela alirejesha na kutoa matusi
kwa hasira.
Ilikuwa hivi, abiria huyo alikuwa miongoni mwa abiri wengi
waliokuwa wanasubiri usafiri katika kituo hicho. Baada ya daladala
tofauti kupita kituoni hapo ikaja daladala moja iliyokuwa imetoka Ubungo
kuelekea Temeke, bila shaka alikuwa anasubiri usafiri huo uliomchukua
yeye na abiria wengine muda kufika kituoni ikiwa na nafasi ya wao
kupanda.
Kutokana na kuwawepo abiria wengine ndani ya
daladala ile, ilimlazimu abiria huyo pamoja na wenzake kugombania
usafiri huo kwa nguvu kama ilivyozoeleka kwa usafiri wa daladala hasa
majira ya jioni na asubuhi.
Katika harakati hizo kuliwa na abiria na wale
majamaa waliozoeleka kuwa ni wapiga debe, lakini kumbe wengi wao ni
vibaka.Wakati wa kupanda daladala baadhi hujifanya kuendelea kupiga debe
na wengine wakijumuika na abiria kupanda daladala. Ndivyo ilivyokuwa
hapo.
Bila ya kufahamu hili wala lile jamaa akawa
anagombea kuingia kwenye daladala mmoja wa vibaka hao wakiwa ameshachora
ramani ya kumwibia. Wakati wa purukushani hizo yule kikaba alifanikiwa
kumchomolea kitu ambacho alidhani ni hela.
Kwa kuwa nia yake ilikuwa ni kuingia ndani ya
daladala hakuwa na wasiwasi wowote hivyo hata hakujitizama ndani ya
mifuko yake. Akasimama akisubiri daladala ianze safari yake. Jambo la
kushangaza ni wakati ile daladala imesimama kusubiri magari yaliyokuwa
yamesimama mbele yake kutokana foleni yasogee, yule kibaka alirejeja na
kurusha vile vitambulisho ndani ya daladala na akitoa matusi na
kufyonza.
Hali hiyo iliwapelekea abiria wa daladala kila
mmoja kutahamaki.Kila mmoja alianza ‘kujisachi’ ndani na mifuko na
mikoba kwa upande wa wanawake. Ndipo yule jamaa akagundua kuwa alikuwa
ameibiwa vitambulisho vyake na kuviokota.
Abiria mwingine wa kike naye aligundua kuwa mkoba
wake ulikuwa umeanza kuchanwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali mithili
ya wembe na kuanza kutoa matusi ya kumtukana aliyejaribu kufanya kitendo
hicho.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa kundi hilo ni kubwa
hivyo mtu akijaribu kumdhuru mmoja wao hupanga njama ya kulipa kisasi
kwa yeyote aliyehusika na jambo hilo.
Post a Comment