Tarime. Waziri ya Mambo ya Ndani, Mathias
Chikawe amesema hatamvumilia askari yeyote anayefanya kazi kinyume na
taaluma yake, badala ya kuwalinda wananchi na mali zao.
Chikawe alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya
siku moja wilayani Tarime juzi, ikiwa na lengo la kujionea hali halisi
yamalalamiko yaliyopelekwa kwake na kupitia wabunge.
Alisema wizara yake imedhamiria kuwashughulikia
polisi wanaowanyanyasa wananchi, ili kurejesha imani ya raia wanaoumizwa
kila siku na kubambukiwa kesi.
“Wizara yangu haitavumilia askari yeyote
atakayefanya kazi ya kubabaisha, tunataka polisi wote wafanye kazi yao
kitaaluma... hatuwezi kuwa askari ambao ni wahalifu,” alisema Waziri
Chikawe.
Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema hayo baada ya
kupata taarifa kutoka wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa African
Barrick Gold North Mara Nyamongo kuwa, kazi inayofanywa na polisi siyo
ya ulinzi bali ujambazi.
Waziri Chikawe alisema kwamba yeye siyo mtu wa
maneno bali vitendo, hivyo wategemee kuona wanaokiuka maadili ya kazi
yao wakiwajibishwa kama ilivyoanza mikoa ya Shinyanga na Mara.
“Mimi siyo mtu wa maneno, bali ni vitendo na
mtaona tayari baadhi ya wale wanaonekana kwenda kinyume na maadili hatua
za kisheria zimeanza kuchukua mkondo wake,” alisema.
Licha ya tuhuma hizo, wananchi waliitupia lawama
Serikali kwa kuwatelekeza bila kuwawekea miundombinu mizuri kwa ajili ya
kutatua matatizo na migogoro inayoibuka kwenye jamii.
“Mwekezaji hana tatizo, maana wakati mwingine
anafanya kazi za kujitolea, Serikali ndiyo imewatelekeza wananchi kwa
kuwaacha wahangaike huku wakituhumiwa kuwa wanafichwa vigumu,” alisema
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangoto, Elisha Nyamohanga.
Alisema viongozi wa ngazi za juu wanafanya ziara bila kushirikisha viongozi wa ngazi ya chini.
, hali inayosababisha wasipate kwa uhakika kero za wananchi.
“Hatukupata taarifa ya ujio wako hapa tumeshtushwa
tu hapa, hakunadiwani, wenyeviti wa vitongoji na vijiji hata mbunge
hatumwoni hapa,hali inayotuonyesha kuwa hamtujali,” alisema Nyamohanga.
Nyamohanga alitoa wito kuwa, ili kupunguza matatizo
yaliyopovijiji vinavyozunguka mgodi huo Serikali iandae maeneo kwa
wachimbaji wadogo na kuwapa vitendea kazi.
“Tatizo la mauaji hapa Nyamongo halitaisha iwapo
Serikali haitaonaumhimu wa kuwapa wachimbaji wadogo maeneo yao,
kwaniwanategemea uchimbaji wa dhahabu kama sehemu ya kipato chao,”
alisema. Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema ziara yake haikuwa ya
utekelezaji, bali ni kujifunz kuona kile kinachomfikia ofisini ajue
sehemu ya kuanzia.
Post a Comment