Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja
wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya
wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo
wenye itikadi kali za kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.
Maandamano yamekuwa yakiandaliwa kila siku kwa
kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kuishinikiza serikali kutia bidii zaidi
katika juhudi za kuwakomboa wasichana hao.'Aibu kwa serikali'
Kampeini ya 'Bring back our Girls, au warudisheni wasichana wetu,'' ambayo imekuwa ikifanywa nchini Nigeria na hata nje ya Nchi hiyo imeleta aibu kubwa sana kwa serikali ya Nigeria.
Waandamanaji wamekuwa wakikutana hadharani wakiishinikiza serikali hiyo kukoma kuzungumza tu katika vyombo vya habari na badala yake waongeze jitihada na kuhakikisha wasichana hao wamekombolewa.
'Makosa sio ya serikali'
Maandamano yamekuwa yakifanyika Nigeria kuitaka serikali kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara
Kundi hili linatumia nembo 'Release Our Girls Boko Haram'. Wameongeza jina Boko Haram kwa kusudi hapo mwisho.
Polisi sasa wanasema kuwa maandamano haya yanatishia usalama kwa wananchi wa Abuja.
Lakini waandamanaji wanaoendesha kampeini ya 'Bring Back our Girls' sasa wanaona kama hili ni jaribio la serikali kuwanyamazisha na wamewasilisha ombi mahakamani kutaka kutolewe agizo la kuvunja amri hiyo ili waruhusiwe
Post a Comment