Dar es Salaam. Wahandisi na mafundi nchini wameonywa kutokubali
kutumiwa na wanasiasa badala yake wafanye kazi kwa uadilifu na kwa
kuzingatia taaluma zao.
Hayo yalisemwa jana na Rais wa Taasisi ya
Wahandisi Tanzani(IET), Dk. Malima Bundara wakati akitoa mapendekezo
yanayohusu mafuriko nchini na msongamano wa magari katika jiji la Dar es
Salaam.
Dk Bundara alisema wahandisi na mafundi hao
wamekuwa wakijisahau na wakati mwingine kutumiwa na wanasiasa na
kuwataka kutambua nafasi zao kwa sababu wao ni watendaji na wanatumia
utaalamu zaidi.
Alisema si sawa kwa mtaalamu kufanya shughuli zake
kisiasa na kuwashauri kuacha tabia ya kukubaliana na wanasiasa kujenga
majengo kwenye mikondo ya asili ya maji na fukwe za bahari huku wakijua
kufanya hivyo ni kosa kwani kunazuia maji kuingia baharini.
“Wahandisi na mafundi mnatakiwa mfanye kazi kwa
kuzingatia taaluma zenu, mtakapowasikiliza wanasiasa mtakiuka sheria na
kuonekana wenye matatizo kitaalamu,”alisema Dk Bundara.
Akizungumzia wiki ya maadhimisho ya wahandisi
yanayotarajiwa kufanyika Septemba 21 hadi 26 mwaka huu, amesema
yatahamasisha kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulinda
mazingira.
Alisema wanaoishi mabondeni wajue kuzibwa kwa njia za asili za maji kuna athiri.
Post a Comment