Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini
Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa
kuelekea Malawi kwa maziko
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu,
Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania,
aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Post a Comment