WAMILIKI wa shule na vyuo binafsi hapa nchini wameiomba serikali kupunguza gharama za vibali vya wageni wanaokuja kufanya kazi nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo binafsi (TAMONGSCO) Benjamin Nkonya alisema kibali cha mwalimu mmoja ni dola 2,000 za Marekani.
Kwa mujibu wa Nkonya gharama hizo zinapanda kila mwaka kiasi kwamba mzigo wa ada unarudi kwa wazazi na walezi jambo linalowafanya waamini kumsomesha mtoto kwenye shule na vyuo binafsi ni ufisadi.
“Mwaka jana gharama za kibali cha kufanyakazi nchini kwa mwalimu mmoja ilikuwa dola 1,600 mwaka huu;… zinapanda kila mwaka.
“…Aprili 30 mwaka huu tulikutana na Rais Jakaya Kikwete mjini Mbeya tukamweleza kilio chetu lakini hakuna mabadiliko.
“Tumekutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiwa bungeni hali ni ile ile; tunaomba waandishi wa habari mtusaidie,” alisema Nkonya.
Alisema iwapo shule inao walimu watano wa lugha ya Kiingereza mmiliki analazimika kulipa Dola 10,000 za Marekani kwa ajili ya vibali hivyo.
Home
»
KITAIFA
» Wamiliki shule binafsi waiangukia serikali kupandisha vibali walimu wa kigeni $ 2000
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment