Leo naomba tuachane na habari zetu za historia
na utalii. Ninataka kuzungumzia uharibifu wa mazingira kama
nilivyoshuhudia huko Handeni mkoani Tanga katika Kijiji cha Nyasa,
vitongoji vya Kariakoo na Ubungo.
Maeneo hayo yanaendesha shughuli za ufugaji, kilimo na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Awali eneo hilo lilikuwa ni hifadhi ya msitu,
likaondolewa katika hifadhi ya msitu, lakini kwa kweli uchimbaji wenyewe
na ufugaji unaharibu mazingira kwa kasi ambayo kama haitadhibitiwa
mambo hayatakuwa mazuri katika siku za usoni.
Eneo hilo limevamiwa na wafugaji ambao wanalisha
mifugo yao bila kujali kwamba wanaharibu ardhi, uoto wa asili na
kusababisha jangwa. Wanyama hao wanalishwa hovyo, unapowaona utadhani
umekutana na makundi ya nyati katika mbuga za wanyama.
Nilishawahi kuandika wakati fulani kuwa migogoro
kati ya wakulima na wafugaji unatakona na kuendekeza aina ya ufugaji
ambao hauzingatii maarifa na teknolojia ya kisasa.
Tulipowaona ng’ombe hao moja ya wazo ni kuwa
unaweza kuwadhibiti wasiingie kwenye mashamba ya wakulima kama
wanalishwa kwa makundi makubwa ya ng’ombe 300 au zaidi.
Serikali inapaswa kuachana na maneno matupu kuhusu
kuingiza maarifa ya kisasa katika shughuli za kilimo na ufugaji.
Handeni katika msimu uliopita kulikuwa na tatizo la njaa na moja ya
sababu ni kukosekana kwa mvua za kutosha.
Ufugaji wa kuharibu misitu na mazingira ya maji
unaoendeshwa huko hauwezi kuwa rafiki ila kuongeza tatizo lingine ambalo
limekuwapo huko kwa muda mrefu.
Inashangaza sana kwa Serikali kuwa wawekezaji
wakubwa wanapotaka kufanya shughuli za uchimbaji, Baraza la Taifa la
Mazingira (Nemc) linawasimamia, lakini Nemc hiyo hiyo inanyamaza kimya
pale wahusika wanapoharibu mazingira hasa wachimbaji wadogo.
Post a Comment