Kivumbi cha Ligi Kuu Bara kinaendelea tena leo kwa timu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013/14 zitashuka kwenye viwanja saba vya mikoa vya mikoa tofauti kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Macho na masikio ya mashabiki na wadau wengi wa soka nchini yatakuwa kwenye viwanja vya Taifa, Dar es Salaam na Sokoine, Mbeya.
Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wanacheza na timu mpya yenye hamasa kubwa ya mashabiki jijini Mbeya, Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine.
Na Simba itakuwa nyumbani jijini Dar es Salaam dhidi ya timu tishio, Mtibwa Sugar. Mbali na mechi hizo¡¯ mtihani mwingine utakuwa kwa timu zifutazo;
Azam FC na Kagera Sugar ¨C Uwaja wa Kaitaba, Bukoba.
Prisons ya Mbeya na Coastal Union ¨C Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
JKT Oljoro na Rhino ¨C pale jiji la Arusha.
Ruvu Shooting na Mgambo Shooting ¨C Uwanja wa Mabatini.
Ashanti United na JKT Ruvu ¨C Uwanja wa Azam Chamazi.

*Ratiba ya Mechi za leo, Jumamosi (saa 10:00)
Simba vs Mtibwa
Coastal Union vs Prisons
Ruvu Shooting vs Mgambo JKT
JKT Oljoro vs Rhino
Mbeya City vs Yanga
Kagera Sugar vs Azam FC
Ashanti United vs JKT Ruvu.

===
Updates:

LIGI KUU BARA:
Simba 2-0 Mtibwa,
Coastal 0-0 Prisons,
Mbeya City 1-1 Yanga,
Kagera 1-1 Azam,
Ruvu Shooting 1-0 Mgambo,
Oljoro 1-1 Rhino,
Ashanti 0-1 JKT Ruvu.