Katika hali isiyotarajiwa hapo jana bodi ya wadhamini wa kanisa la
Tanzania Assemblies of God nchini jijini Mwanza iliamua kwenda
mahakamani kuwasilisha pingamizi la kutoruhusu mwili wa aliyekuwa askofu
mkuu wa kanisa la E.A.G.T marehemu Dkt. Moses Kulola kuzikwa katika
viwanja vya kanisa hilo lililopo maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakidai
ni mali yao jambo ambalo hata hivyo haikuwezekana na mwili huo utazikwa
kama ilivyopangwa mapema hii leo.
Akizungumza na WAPO Radio Fm kupitia kipindi cha habari Yaliyotokea
askofu Lameck Mkumba wa E.A.G.T amesema ameshangazwa na uamuzi huo
kwakuwa waumini wa kanisa la E.A.G.T wamekuwa wakilitumia kanisa hilo la
Bugando kwa muda mrefu sasa bila kuwapo matatizo yeyote hadi kuibuka
kwa suala hili ambalo hawakutarajia" Mimi mwenyewe nina miaka zaidi ya
15 nikiwa muumini na niliokoka ndani ya kanisa hili la Bugando E.A.G.T"
amesema askofu Mkumba
Aidha askofu huyo amesema baada ya kuona wenzao wametumia taratibu za
kisheria kwakutumia bodi ya wadhamini wao mahakamani ikabidi nao pia
kutafuta uwakilishi wa kisheria ambao uliwasimamia vyema kwakuwasilisha
vielelezo na maelezo ya msingi ambayo mahakama iliridhika nayo nakuamua
kuwapa kibali cha kuendelea na maziko ya askofu Kulola katika viwanja
hivyo.
Kwa
upande wake mchungaji wa kanisa la E.A.G.T City centre la jijini Dar es
salaam Florian Katunzi amesema licha ya changamoto zote za kibinaadamu
zilizojitokeza bado askofu Moses Kulola ataendelea kuwa shujaa wa imani
nchini kutokana na kufahamika kwake vyema katika suala la injili na
kulitaka kanisa kwa ujumla kukaa tayari kwakuwa Yesu anakuja na kuwataka
kuachana na migongano ambayo haisaidii kanisa kusonga mbele.
Wakati huo huo askofu mkuu wa kanisa la T.A.G Barnabas Mtokambali
anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake saa nne
asubuhi leo kwaajili ya kutolea ufafanuzi baadhi ya mambo baada ya
kuulizwa na mtangazaji wa WAPO Radio FM Beatrice Kamanga kupitia kipindi
cha Yaliyotokea akitaka kujua amepokeaje hali iliyojitokeza huko Mwanza
hapo jana.
![]() |
| Hapa ndipo atakapolala Askofu MKuu Moses Kulola |


Post a Comment