0

Matukio ya AfrikaPolisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesambazwa katika maeneo ya Nyiragongo kaskazini mwa Goma, pamoja na viunga vyake maeneo yaliokuwa yanashikiliwa na waasi wa M23 ili kuimarisha usalama zaidi.

Waasi walitoroka huko kufuatia makabiliano makali yaliyodumu wiki nzima kati yao na vikosi vya serikali na majeshi ya Umoja wa Mataifa.
Amina Abubakar amezungumza na Gavana wa Kivu Kaskazini Julien Paluku na kwanza alimuuliza juu ya hali ilivyo kwa wakati huu.Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar

Post a Comment

 
Top