- Luis Suarez (26) anawaniwa na Real Madrid kwa dau la £45m.
- Kiungo mshambuliaji Mesut Ozil (24) huenda akatua Arsenal kwa dau la £42.5m
- Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic sasa yumo kwenye hatihati ya KUONDOKA PSG baada ya kutua kwa Cavani. ManCity na Chelsea wanategemewa kumwaga ofa.
- ManCity sasa wanamwania winga machachari Eduardo Salvio wa Benfica kwa dau la £25.8m.
- Kiungo mshambuliaji Juan Mata (25) anawaniwa na Arsenal.
- Marouane Fellaini (25) anapendelea zaidi kujiunga na ManUtd kuliko Arsenal kama atafanikiwa kuhama. ManUtd wanatakiwa kumwaga £40m ili kumng'oa Everton.
- Beki Patrice Evra (32) ameweka wazi kwamba atarudi Monaco endapo Leighton Baines atasajiliwa ManUtd.
- Beki kiwango Leighton Baines (28) wa Everton anawaniwa na ManUtd kwa dau la £15m.
- Kiungo mshambuliaji Miguel Michu (27) sasa huenda akatua Arsenal kwa dau la £25m.

DONE DEALS (BIG NAME TRANSFERS):

REAL MADRID
- Gareth Bale (24) ametua Real Madrid kwa uhamisho wa £85.3m (REKODI YA DUNIA) kwa mkataba wa miaka 6. Atalipwa mshahara wa £300,000 kwa wiki. Kumbuka Christiano Ronaldo alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la £80m.

MANCHESTER UNITED

- bado bado, mwenda pole hajikwai.

ARSENAL
- Kiungo Mathieu Flamini (29) amerejea Arsenal kutoka AC Milan kwa uhamisho huru. Flamini aliichezea Arsenal mwaka 2004 - 2008.
- Mshambuliaji Gervinho ameuzwa AS Roma ya Italia kwa bei ya £8m.

CHELSEA

- Mshambuliaji Samuel Eto'o (32) ametua Chelsea kwa uhamisho huru kutoka Anzhi Makhachkala, kwa mkataba wa mwaka 1.
- Kiungo mshambuliaji Willian (25) ametua kwa uhamisho wa £30m kutoka Anzhi Makhachkala ya Urusi. Mkataba miaka 5.
- Kiungo Florent Malouda ameondoka Chelsea kwenda Trabzonspor ya Uturuki kwa mkataba wa miaka 2.
- André Schürrle kutoka Bayer Leverkusen ametua kwa dau £18m.
- Marco van Ginkel ametua kutoka Vitesse Arnhem kwa dau la £8m.

LIVERPOOL

- Mshambuliaji wa Chelsea Victor Moses (22) amehamia Liverpool kwa mkopo wa msimu mmoja.
- Beki wa kati na kushoto Mamadou Sakho (23) ametua Liverpool kwa dau la £18m kutoka PSG.
- Beki wa kati Tiago Ilori (20) ametua Liverpool kutoka Sporting Lisbon kwa dau la £7m.
- mshambuliaji Iago Aspas ametua kutoka Celta Vigo kwa dau la £7m.
- Golikipa Simon Mignolet ametua kutoka Sunderland kwa dau la £9m.
- Beki Kolo Toure (32) ametua Liverpool kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Jamie Carragher kustaafu.
- Kipa Pepe Reina ameondoka Liverpool na kutua Napoli kwa mkopo. Anaungana tena na kocha Rafa Benitez.
- Mshambuliaji kinda Jonjo Shelvey ameondoka Liverpool kwenda Swansea kwa dau la £5m.
- Mshambulaji Andy Carroll amehamia West Ham kwa dau la £15.5m

MANCHESTER CITY
- Beki Martin Demichelis (32) ametua ManCity kwa dau la £3.5m kutoka Atletico Madrid.
- Mshambuliaji Stevan Jovetic (23) ametua kwa dau la £22m kutoka Fiorentina.
- Mshambuliaji Alvaro Negredo (27) ametua kutoka Sevilla kwa dau £20m.
- Beki Maicon (31) ameondoka ManCity kwenda AS Roma, baada ya kucheza mechi 13 tu tangu ajiunge na City.
- Fernandinho ametua kutoka Shakhtar Donetsk kwa dau la £30m.