Kumekua na wasiwasi wa ID
Privacy kuhusiana na maamuzi ya kampuni kubwa ya Teknolojia Apple
kuzindua Teknolojia ya Fingerprint kwa ajili ya kuifungua loki [unlock]
simu hio, mjadala huo umetokea kwasababu wadau mbali mbali wa matumizi
ya teknolojia kuhofia utambulisho wao/ID kuhifadhiwa na kutumika katika
maswala ya ujasusi/spying.
Lakini kampuni hio ya Apple imesema kwamba
toleo lao hilo jipya la iPhone 5s haitakua ikihifadhi utambulisho wa
alama za viganja/vidole katika simu hizo na kuwa wasiwe na wasiwasi kwa
kua wanaheshimu na wanatambua umuhimu wa usiri/Privacy wa wateja wao.
Pia wamesema Teknolojia hio inachukua tu baadhi ya alama za vidole na
ambayo ni simu peke yake ndo itaweza kumtambua mtumiaji wake, na pia
Kampuni ya apple imesema kwamba teknolojia hio haitakua ikifanya kazi
kwa ufasaha mda wote na hio nimoja ya udhaifu wake na pia haitakua na
uwezo wa kusupport program nyingine zaidi ya za Apple tu.

Post a Comment