Kama iilivyo ada katika mwendelezo wa masomo yetu hapa kwa blogg yetu, tunaendelea na somo letu namna ya kutumia Brush Tool katika Software ya Adobe Photoshop Cs 5. Kama ni mara ya kwanza kufuatilia masomo yetu hapa Fm Graphics tulianza na somo la kwanza na tulianza kufundisha namna ya kutumia MOVE TOOL ambayo ndiyo tools ya kwanza katika software yetu.
Katika somo lililopita nilisema nitazungumzia mambo kama 4 hivi katika tool hii
A:MAANA YA NENO BRUSH KATIKA SOFWARE YETU
B: NAMNA YA KUHIFADHI BRUSH [BRUSH INSTALLATION]
C: DOWNLOAD AINA YA BRUSH UNAYOITAKA KATIKA MATUMIZI YAKO
{nitatoa link ya kudownload free brush.}
D:MATUMIZI YA BRUSH KATIKA PICHA
Na katika somo lililopita nilizungumzia zaidi maana ya neno Brush. BRUSH- Hii ni tool ambayo inatumika katika uchoraji ndani ya sofware yetu, kwa lugha nyingine tunasema Basic painting tool na ina patikana katika Tools Bar, Shortcut yake ni herufi B katika key board yako (The Brush tool is a basic painting tool. It works like a traditional drawing tool by applying the color using strokes. It’s located in the standard Tool Bar and its default shortcut is the letter B). Kama tunavyoiona katika Tools palett yako hapo chini.
Pia tuliangalia mpangilio wa Brush katika tools pallet yeko kama ifuatavyo
Bila kupoteza mda tungie kwenye kipengele cha pili
B: NAMNA YA KUHIFADHI BRUSH TOOL YAKO(BRUSH INSTALLATION)
Hapa kuna hatu ambili za kuhifadhi Brush tool yako pindi unapoipakuwa tu kutoka kwenye mtandao
NJIA YA KWANZA:
1. Download brush yako kutoka katika mitandao mbalimbali( nitatoa link ya kudownload brush hapo baadaye) Extension yake ni "ABR"
A:Kwa wanaotumia (Mac)- /Users/{username}/Library/Application Support/Adobe/Adobe Photoshop CS5/Presets/Brushes
B:Kwa wanaotumia (Windows) C:\Program Files\Adobe\Photoshop\Presets\Brushes
Hapo utakuwa umefanikisha hatua ya kwanza ya kuhifadhi Brush katika sofware yako
NJIA YA PILI:
- Fungua sofware yako ya Adobe Photoshop, bonyeza latter “B”
kwenye keyboard yako ili kuactive brush yako. Sasa nenda kwenye Option
Palette yako kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
- Baada ya hapo bonyeza Triangle iliyo kulia kwako kama inavyoonekana katika picha yako
- Utaona kwa chini neno ‘Load Brushes’ bonyeza hapo
baada ya kubonyeza tu itakudirect moja kwa moja Sehemu ulipohifadhi Brush zako "abr" file. Then bonyeza Load
Natumaini umenielewa katika uhifadhi wa Brush Tool (BRUSH INSTALATION) katika Sofware yetu.
C: DOWNLOAD BRUSH KATIKA MITANDAO HII BURE
1-myphotoshopbrushes
2:all-free-download.com
3:brusheezy.com
Ipo mitandao mingi sana inayotoa Brush lakini natumaini hii mitatu itakuwezesha kufanikisha zoezi lako.
NATUMAINI TUMEELEWANA KATIKA SOMO LETU LA LEO, KAMA NI MARA YAKO YA KWANZA KUFUATILIA MFULULIZO WAMASOMO YETU HAPA FM GRAPHICS ILI KUPATA MAELEKEZO YA MASOMO YALIYOPITA LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK NA TUTAKUELEKEZA MAHALI PA KUYAPATA.



