Dar es Salaam. Wakati Yanga na Azam zikiingia kambini rasmi jana
kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii, nyota wa Jangwani,
Hamis Kiiza ameanza rasmi mazoezi na kutoa ahadi ya kuipa timu hiyo
ubingwa.
Yanga imejificha kwenye Hoteli ya Protea kujianda kuwakabili washindi wa pili mfululizo wa Ligi Kuu Bara.
Kocha Ernie Brandts amefurahi kurejea kwa nyota
huyo wa Uganda na kusema kutasaidia timu yake kufanya vizuri kwenye
mechi ya Jumamosi.
Kiiza alifanya mazoezi na wachezaji wenzake kwenye
Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam. Kiiza alisema:
“Nimerudi rasmi kuanza kazi, hii ni timu ninayoipenda.”
“Kila mchezaji ana lengo, lakini kubwa ni kuhakikisha Yanga inakuwa bingwa tena msimu huu,” alisema zaidi. Kwa upande wao,
Azam FC imeingia rasmi kambini kujiandaa na mchezo
wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Jumamosi wiki hii kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinaingia kambini baada ya kuwasili
kutoka nchini Afrika Kusini ilikokwenda kuweka kambi, ambapo walicheza
mechi nne, ikipoteza dhidi ya Kaizer Chiefs, Orlando Pirates, Moroka
Swallows na kushinda moja dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Post a Comment