0

 
Hivi karibuni kumekuwa na midahalo mbalimbali ambayo imekua ikiendelea katika nchi nyingi, ikiwamo Tanzania kuhusu masuala ya ulinzi wa huduma za mtandao.
Binafsi nimepata kuhudhuria mijadala kama mwanachama wa kudumu wa kikundi kinachojihusisha na masuala ya ulinzi mtandao katika nchi za Afrika.
Katika vikao tofauti, majadiliano yalikua ni mengi ambapo hali ya usalama wa kimtandao imechambuliwa kwa ngazi ya kidunia, na kudhihirika kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la makosa ya kimtandao, hususan mwaka huu.
Hadi sasa baadhi ya nchi tayari zimeweza kupiga hatua katika kukabiliana na hali hiyo. Taarifa iliyowasilishwa na Profesa Hamadoun Toure kutoka ITU (International Telecommunication Union) iliyo chini ya Umoja wa Kimataifa ilisema, kuna mategemeo mwishoni mwa mwaka huu pakawa na watumiaji biilioni 2.7 wa mtandao
Aidha, ripoti iliyowasiilishwa na ITU huko Geneva ilisema, kumekuwepo na ongezeko kubwa la madhara ya uhalifu wa kimtandao, ambapo ilielezwa mitandao imekuwa ikiathiriwa kwa zaidi ya asilimia 30.
Pia mitandao ijulikanayo kama “Phishing Sites spoofing social networks” imeongezeka kwa asilimia 125, na kuelezwa nusu ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 uliimwenguni kote wamekua wakiathirrika na kilichotambulishwa kama “Cyberbulling”.
Vile vile tafiti zilizowasilishwa katika ripoti ya “The World Federation of Exchanges and the International Organization of Securities Commissions” zimeeleza nusu ya taasisi za fedha duniani zimeweza kuathirika na uhalifu wa kimtandao ikiwamo wizi hadi kufikia mwaka jana mwishoni
Kibaya zaidi ni kwamba takriban robo ya taasisi hizo zinaelezwa kushindwa kutatua changamoto hiyo.
Kimsingi, jambo hili na mengine yaliyojadiliwa kwa kina yalionekana kuwa ni changamoto kubwa katika dunia ya sasa, ambapo kutakuwa na ugumu mgumu kukimbia utumiaji wa teknolojia katika maisha ya kila siku.
Hali ilivyo Tanzania
Kwa sasa hali ya utumiaji wa mitandao nchini imeongezeka katika sekta mbalimbali, kuanzia kufanya miamala ya biashara hadi katika sekta za elimu na maeneo mengine mengi.

Post a Comment

 
Top