Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)