Ni fedha zinazoidiwa kulewa wakati wa mkutano wa kimataifa uliofanyika jijini Dar es Salaam
Patricia Kimelemeta, Mwananchi
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali(CAG, Ludovick Utouh, amesema kuwa atafanya ukaguzi maalumu
wa kashfa ya wizi wa Sh8 bilioni zilizotumika katika mkutano wa Smart
Partnership Dialogue.
Mkutano huo ambao ulifanyika Dar es Salaam kuanzia
Juni 28 hadi Julai Mosi mwaka huu ulindaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa hivi karibuni, ulihusisha viongozi wakuu wa
Afrika.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam
jana, Utouh alisema kuwa, ukaguzi wa fedha hizo utaanza kufanyika Oktoba
mwaka huu, huku ukienda sambamba na ukaguzi wa matumizi za wizara hiyo
kwa mwaka wa fedha 2013/14.
“Tutafanya ukaguzi maalumu wa Sh8 bilioni
zilizotumika katika mkutano wa Smart Partnership Dialogue ili tuweze
kubaini matumizi ya fedha hizo,”alisema Utouh.
Aliongeza, kwa mujibu wa sheria, CAG anapaswa
kukagua matumizi ya fedha zote za Serikali zinazotumika katika Wizara,
Taasisi na Mashirika ya Serikali ili waweze kubaini uhalali wa matumizi
ya fedha hizo kwa kila ibara.
Alisema, kwa sasa zoezi la kufunga hesabu
linafanyika Septemba mwaka huu, kila wizara ikiwamo Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa zitatakiwa kuwasilisha taarifa hizo
ofisini wake kwa ajili ya kuanza ukaguzi ambao utafanyika Oktoba mwaka
huu.
“Kwa sasa wizara nyingi ikiwamo Wizara ya Mambo ya
Nje inakamilisha zoezi la kuhakiki hesabu zao, na kwamba wakimaliza
wanatupa taarifa ili tuweze kukagua hesabu zao za mwaka, jambo ambalo
linaweza kutusaidia kubaini matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa
mwaka,” aliongeza.
Aliongeza ikiwa fedha hizo zimetumika kinyume na
taratibu, zitabainika na kwamba watawalisha taarifa hiyo serikalini kwa
ajili ya kuwachukulia hatua watu watakaobainika wametumia vibaya fedha
za Serikali.
Post a Comment