Kwa mara nyingine tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa.
Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya.
“Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.” P funk
Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema:
“Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm.
Sababu
kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita number one radio
station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka.
Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.”
Mimi cha kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingie kwamba bila nyinyi
tutaweza. Cha pili mnaingiza hela sana ya wadhamini lakini
hamui-distribute kwa wanaohusika…

Post a Comment