Mlipuko mkubwa umetokea leo mbele ya lango kuu la Kituo cha UN mjini
Garowe ambako ulilengwa Gari waliokuwemo Wafanyakazi wa kigeni wa UN.
Taarifa
zaidi zinaeleza kuwa Mlipuko huo ulilengwa Gari aina ya Mini Bus
inayomilikiwa na Umoja wa Mataifa ambako walikuwemo karibu wafanyakazi
20 wa umoja huo na inaarifiwa waliopoteza maisha wamefikia watu 10
wakiwemo wafanyakazi wa kizungu na waafrika kutoka Uganda na Kenya huko
idadi ya waliojeruhiwa ikifikia watu 7.
Taarifa
iliyotolewa na Mujahidina wa Al-Shabab ilithibitisha kuwa wao ndio
waliotekeleza shambulio hilo na kuwalenga wafanyakazi wa UN huko
wakithibitisha vifo vya watu 10 wengi wao wakiwa ni wafanyakazi wa
kigeni na idadi nyingine ya Majeruhi.
Mpaka
sasa Mujahidina hawajafafanua namna ulivyofanyika shambulio hilo,picha
kadhaa iliyochukuliwa Gari iliyolengwa zilionyesha uharibifu upande wa
juu wa Gari hilo.
Post a Comment