Serikali ya Somalia imetangaza ruzuku ya dola milioni moja kwa yeyote atakayeisaidia kuwakamata viongozi 11 wa Al Shabaab.
Orodha hiyo ya watu 11 wanadaia kuwa viongozi wa ngazi ya juu ya katika kundi hilo la wapiganaji wa wa kiislamu wa Al shabaab.
Kiongozi
wa kundi hilo la wapiganaji Ahmed Diriye anaongoza katika orodha hiyo
huku Serikali ikitoa ruzuku ya dola laki mbili u nusu ($250,000) kwa
yeyote atakayetoa habari zitakazofichua aliko.
Kitengo cha wanawake cha Al Shabaab
Jumla ya dola milioni moja zimetengwa katika hatua hii ambayo inalenga kuchochea umma kuisaidia serikali hiyo kuitokomeza
kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa nchini kenya. Orodha
Kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa nchini kenya
Al Shabaab ambayo imetangaza wazi kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda wameahidi kuendelea
kuishambulia Kenya hadi serikali hiyo itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa wanajeshi wa muungano wa Afrika .
Kundi hilo linataka Kenya iondoe majeshi yake nchini Somalia
Majeshi ya Muungano huo inashikilia maeneo mengi ya mijini kwa ushirikiano na majeshi ya Serikali ya Somalia huku
kundi
hilo la Al Shabaab ikitawala maeneo ya mashambani kusini mwa taifa
hilo ambalo limekuwa bila serikali kwa zaidi ya miongo miwli sasa.
Post a Comment