Eminem ameigiza pia kwenye filamu ya The Interview ambayo
imekuwa chanzo cha kukua kwa mgogoro kati ya Marekani na Korea
Kaskazini.
Kuonekana kwa Eminem kwenye filamu hiyo kunaweza kuwa kunachekesha
zaidi kwa wengi pale ambapo rapper huyo anayefahamika kwa mashairi yake
ya kuwaponda mashoga akimshangaza mtangazaji (nafasi iliyoigizwa na
James Franco) aliposema kuwa naye ni shoga.
Kauli ya Eminem ilionekana kumwacha mdomo wazi mtangazaji huyo ambaye alionekana kutoamini alichokisikia.
Filamu ya The Interview ilisitishwa kuzinduliwa kwenye majumba ya
sinema nchini Marekani siku ya Christmas baada ya hackers kutishia
kufanya shambulio la kigaidi kama lile la September 11.
Badala yake kampuni ya Sony iliamua kuizindua filamu hiyo mtandaoni
na hadi sasa imeshaingiza zaidi ya dola milioni 15 na kufanya kuwa
filamu ya kampuni hiyo iliyowahi kupakuliwa zaidi mtandaoni.
Home
»
KIMATAIFA
» Eminem ameigiza kwenye filamu ya ‘The Interview’ ambamo alijitangaza kuwa ni shoga (Video)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)