0
Vanessa Mdee amesema kuwa pamoja na kuwa na orodha kubwa ya wasanii wa Afrika anaowasilia nao nao kwenye simu, hajafirikia kufanya collabo kwakuwa bado hajapata wimbo muafaka.
VANESSA
Vanessa aliiambia Bongo5 kuwa sio kila collabo inaweza kufanya vizuri kwakuwa inategemea na ‘chemistry’. “Mtu unaweza ukaingia naye studio ukajuta sababu ulifanya papara kumshirikisha. Inabidi utumie muda kuamua,” alisema.
Muimbaji huyo alitolea mfano maongezi aliyofanya na Diamond kuhusu kufanya wimbo pamoja lakini bado hawajapata wimbo unaowafaa wote kwa pamoja. Diamond na Vanessa wote wametajwa kuwania tuzo za AFRIMA 2014 zitakazotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria.

Post a Comment

 
Top