0
Fareed Kubanda a.k.a Fid Q amesema anatarajia kwenda nje ya nchi kushoot video yake mpya. Rapper huyo wa Rock City amesema amedhamiria kuanza kufanya video nzuri baada ya kukaa muda mrefu bila video nzuri au wakati mwingine kutofanya kabisa licha ya kutoa hits nyingi.
Fid q
“Nimedhamiria kufanya video nzuri, kwahiyo kiukweli nashindwa kusema itakuwa ni aina gani ya video lakini nachoweza kusema ni kwamba itakuwa ni video nzuri kwasababu sina video nzuri.” Amesema Fid Q kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm, aliongeza “Na hizi setbacks nyingi za Fid Q zimetokana kwamba Fid Q anatoaga ngoma kali kila siku lakini huwa hafanyi videos.”
Hata hivyo Fid ameiambia Bongo 5 kuwa kwasasa asingependa kusema ataenda kushoot nchi gani wala director atakayemtumia, “unajua swala la video mpya uongozi bado haujaruhusu nifunguke zaidi, tumegundua kwamba kuongea bado muda hatufanyi, kwahiyo tukasema kwamba tufanye halafu tutawatangazia kwamba hii kitu imefanyika sehemu hii na inatoka siku hii”.
Fid pia ametoa sababu zilizokuwa zinamfanya asizifanyie video ngoma zake,

“Kwanini nataka nikafanya video, nataka nikafanye video kwasababu kwanza nilikuwa sifanyi video kwasababu nilikuwa naona kumbe video zipo kwaajili ya kufanya track I-hit. Kwahiyo mimi nikawa mtu ambaye nauwezo wa kutengeneza ngoma na ika hit bila kufanya video, uwezo ambao sio kila msanii anao.”

Aliendelea, “Lakini research ambayo nimeifanya hivi karibuni nimegundua kwamba video sio tu kwamba inaweza ikasababisha ngoma ika hit, video inasaidia pia kukujenga wewe msanii na brand yako kwa ujumla…watu wanakuwa wanapata ukaribu na wewe zaidi wewe na sanaa yako zaidi, kuliko wanavyokuwa wanakuskia tu kwenye audio na ku imagine huyu jamaa anakaa hivi anakaa hivi, yaani its like you are talking to him.”

Post a Comment

 
Top