0
Mastaa wawili wa R&B, Chris Brown na Trey Songz wote kutoka Virginia, Marekani, baada ya kutease kwa muda mrefu hatimaye Jumatatu ya wiki hii wametangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa tour yao ya pamoja.
Chris n Trey
Breezy na Songz wanatarajia kuanza tour yao waliyoipa jina la ‘Between The Sheets’ January 28, 2015.
Katika show yao ya kwanza itakayofanyika Hampton,mgeni maalum anatarajiwa kuwa Tyga.
Maeneo mengine ambako Breezy na Songz wataenda ni Brooklyn, Atlanta, Detroit, Toronto , Washington na kumalizikia Los Angeles March 8.

Post a Comment

 
Top