Akiongea kwenye kipindi cha Kili Chat kinachorushwa kila Alhamis kupitia EATV, Ben Pol alisema show yake mbaya zaidi kuifanya ni ile ya kwanza kabisa kuwahi kufanya wakati huo akiwa na wimbo uliomtambulisha, ‘Nikikupata’.
“Nafikiri pia sababu ya ugeni wa jukwaa, nilikuwa na wimbo mkubwa ‘Nikikupata’ ilikuwa imeshaanza kufanya vizuri, video yake na nini,” alisema Ben. “Lakini nilikuwa sijafanya show na ile ilikuwa ni show yangu ya kwanza. Nadhani pia nilikuwa nimepooza. Kwahiyo watu walikuwa hawarespond kabisa, kama wanataka show iishe,” aliongeza.
Ben Pol alisema kingine ni kwasababu alikuwa na wimbo mmoja tu hivyo hakuwa na nafasi ya kurekebisha makosa kwa kuimba wimbo mwingine.
Post a Comment