0
Orodha ya kwanza ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara 2015 imetoka.
Tarabband_(Sweden/Iraq/Egypt)_Sauti_za_Busara_2014_(photo_Peter_
Tamasha hilo lililotajwa na CNN International miongoni mwa matamasha 7 muhimu barani Afrika litafanyika visiwani Zanzibar February 12 – 15, 2015. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Amani na Umoja’ na litajikita zaidi kwenye muziki wa Tanzania.
OCTOPIZO (532x800)
Octopizzo

Kundi la Weusi na rapper wa Kenya, Octopizzo ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.
weusi gere
Makundi mengine ni pamoja na:
Culture Musical Club, Mim Suleiman, Msafiri Zawose, Weusi, Leo Mkanyia & Swahili Blues Band, Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta, Mgodro Group, Zee Town Sojaz, Rico Single & Swahili Vibes, Ifa Band, Mwahiyerani na Tunaweza Band.
Mengine ni Mabantu Africa, Cocodo African Music, Kiki Kidumbaki, DCMA Young Stars, Shirikisho Sanaa Group, Babawatoto Centre na mengine. Kutoka Kenya pamoja na Octopizzo, Sarabi na Bonaya Doti watatumbuiza na Rwanda ni Liza Kamikazi na bendi yake.

Post a Comment

 
Top