0

Wakati ambapo wasanii mbalimbali wa Tanzania wamekuwa wakizungumza kuhusu kutumia kiasi kikubwa cha fedha kugharamikia video zao za muziki, Vanessa Mdee anatarajia kuingiza mkwanja mrefu kutokana na video ya wimbo wake ‘Hawajui’.

Vanessa ameiambia Bongo5 exclusively kuwa kuna kampuni ambayo itamlipa fedha kupachika bidhaa yake kwenye video ya wimbo huo kama njia ya kujitangaza. Katika masoko kitu hicho kinaitwa ‘Product Placement’ ambapo kampuni inamlipa msanii kwa kutangaza bidhaa yake kwenye video yake ya muziki. Hicho sio kitu kigeni kwa nchi zilizoendelea kama Marekani ambapo bidhaa kama Beats by Dre au kilevi cha Ciroc zimekuwa zikionekana kwenye video za wasanii kibao wa huko.
“Nataka kuwaonjesha kitu, labda niwape exclusive Bongo5,” alisema Vee Money. “ Unajua product placement? The concept ya product placement .. unatia product ya brand kubwa kwenye video yako halafu wanalipia. That’s what I am saying, wait for it, it’s gonna be great,” alisema Vanessa ambaye hakutaka kuitaja brand hiyo.
Kutokana na wateja wengi kutopenda kuyaangalia matangazo, makampuni yamekuwa yakitafuta njia nzuri ya kujitangaza ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012, makampuni yalitumia zaidi ya dola bilioni 8.25 kwaajili ya ‘product placement’ duniani kote.

Post a Comment

 
Top