Oscar na Reeva
Pistorius alihukumiwa miaka mitano jela kwa kumuua Steenkamp bila kukusudia. Alidai alimpiga risasi kupitia mlango wa choo nyumbani kwake Pretoria, February 14, 2013, akidhania ni jambazi.
Gazeti la Sunday Times limeandika kuwa June Steenkamp ameandika kwenye kitabu chake kuwa haamini story hiyo Pistorius. “Alisema kuvuta trigger ilikuwa ajali, Nini? Mara nne ni ajali? Alisema Reeva hakupiga kelele, lakini nina uhakika alipiga kelele. Namjua binti yangu kwakuwa alikuwa na sauti sana,” ameandika kwenye kitabu hicho.
“Hakuna shaka kwenye fikira zetu kuwa kitu kibaya kilitokea, kitu kilichomuudhi Reeva kiasi cha kujificha nyuma ya mlango uliofungwa na simu mbili za mkononi.”
Post a Comment