0
Mara nyingi baadhi ya watu waliokuwa wapenzi wanapoachana huamua kurudisha baadhi ya vitu walivyopeana walipokuwa wapenzi kwa sababu mbalimbali, kitu ambacho muimbaji Jordin Sparks pia amepanga kufanya.
sparks2
Sparks alikuwa mgeni kwenye kipindi cha ‘Wendy Williams Show’, na miongoni mwa maswali aliyokutana nayo ni pamoja na kuhusu habari za kuvunjika kwa uchumba wake wa miaka 3 na Jason Derulo.
sparks
Pamoja na kuwa hakutaka kuzungumzia sababu za kuachana lakini aliweka wazi mpango wake wa kutaka kumrudishia Derulo gari aina ya BMW aliyompa kama zawadi wakati wa Christmas December mwaka jana .
“I haven’t really had time to think about it, but yeah, I probably will..He can have it.” alisema

Post a Comment

 
Top