Muimbaji huyo mwenye 45, mwenye watoto mapacha Max na Emme wenye miaka sita aliowapata kwenye ndoa yake na Marc Anthony anasisitiza kuwa kuona wanae wanahisi kupendwa ni kitu cha muhimu zaidi katika maisha yake lakini hilo halijawazuia marafiki zake wanaotaka kumkutanisha na mwanaume mwingine.
“Marafiki zangu wanajaribu mara nyingi kuniunganisha lakini sipo huko kwa sasa. Sio kitu ambacho nimekipa kipaumbele,” ameliambia gazeti la Daily Mirror.
“Sasa hivi najisikia vizuri kuwa peke yangu na kuwa na muda wa ‘I love Jennifer’ ambao sijakuwa nao sana katika maisha yangu. Natumia muda mwenyewe na wanangu. Nataka watoto wajue kuwa wanapendwa, hicho ndio kitu cha muhimu. Kuwa mama ni kipaumbele changu cha kwanza.”
Post a Comment