0
Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola unaweza kuzigharimu nchi za Afrika Magharibi zaidi ya dola bilioni 52 katika mwaka ujao iwapo maafisa watashindwa kuudhibiti, benki ya dunia imeonya.
ebola-virus-close
Benki hiyo imesema kwenye ripoti yake mpya kuwa, kama jitihada za kuzuia kusambaa kwake katika nchi zilizokubwa zaidi na ugonjwa huo– Liberia, Sierra Leone na Guinea – hazitafanikiwa hadi December, nchi hizo zitakabiliwa na tatizo kubwa la kiuchumi.
Milipuko midogo ya ugonjwa huo kwenye nchi za Nigeria na Senegal imedhibitiwa, benki hiyo imesema.
Hadi sasa Ebola imeua watu 3,500.

Post a Comment

 
Top