0
Rapper mkongwe na mtangazaji wa redio, Soggy Doggy amesema yupo mbioni kuachia ngoma mpya na wasanii wakongwe wenzie, Juma Nature, Inspekta Haroun, Suma G na Hammer Q.
soggy-3
Soggy ameiambia Bongo5 kuwa ngoma hiyo imetayarishwa na Q the Don.
“Tangu nimerudi kuishi Dar nimeshaenda studio za Majani sana. Zaidi ya muziki natarajia zaidi kurekodi lakini kuna vitu vingine navyo nilikuwa najadili na Majani vya kutengeneza mkwanja. Uzuri nafanya kazi kwenye radio, kuachia ngoma ni kitu cha kawaida. Nitaendelea kuachia ngoma kali kama kawaida. Na kwa kuanzia tu kuna ngoma ambayo tulifanya Mwanza kama miezi mitatu iliyopita nimefanya mimi, Juma Nature, Inspekta Haroun, Suma G pamoja na Hummer Q, tunajiita ‘Way Back’. Kuna ngoma tulitengeza na Q the Don ambayo tunaweza tukaiachia wiki mbili, tatu zijazo. Kwahiyo kuna mambo makubwa yanakuja.”
Sikiliza teaser ya wimbo huo hapa.

Post a Comment

 
Top