Kampuni inayoongoza kwa mawasiliano nchini Vodacom Tanzania na
kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola Tanzania wamezindua promosheni ya Coke
Studio itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kupata dakika 5 za
maongezi
wanapokunywa soda ya Coke ambapo mteja atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye namba zilizopo chini ya kizibo kwenda namba 15441.
wanapokunywa soda ya Coke ambapo mteja atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye namba zilizopo chini ya kizibo kwenda namba 15441.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twisa akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Coke Studio msimu wa pili ambapo wateja wa Vodacom Tanzania watajipatia muda wa maongezi wa dakika tano bure kwa kila soda moja ya chupa ya Coca-Cola
Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika jijini Dar es
salaam Meneja wa Kinywaji cha Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka
amesema ”promosheni hii ni katika kuhakikisha kwamba vijana na wateja
wote kwa ujumla wanapata nafasi ya kuburudika na kinywaji cha Coca-Cola,
lakini pia kuweza kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi kwenye
intaneti kwa muda wa dakika 5”
Naye Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania
Kelvin Twissa akizungumza katika uzinduzi huo amesema promosheni hii
inayojulikana kama Kunywa Coke #Kula5 ina lengo la kuwafurahisha wateja
wa Vodacom
Tanzania na wenzao wanaowazunguka.
Tanzania na wenzao wanaowazunguka.
“Mteja atakuwa anafurahia kunywa Coke wakati huo pia anapata fursa ya kutumia huduma za mtandao kwa dakika 5 kwa
namna yoyote anayotaka yeye (mteja) ikiwa ni kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kuperuzi’’
namna yoyote anayotaka yeye (mteja) ikiwa ni kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kuperuzi’’
“Mteja wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe
wenye namba iliyopo chini ya kizibo cha soda yake ya Coca-Cola ya chupa
kwenda namba 15441 bila kutozwa gharama yoyote na baada ya hapo atapokea
ujumbe wa
uthibitisho kwamba ana dakika 5 kuanzia muda huo kutumia kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi.”
uthibitisho kwamba ana dakika 5 kuanzia muda huo kutumia kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi.”
Kupitia promosheni hii wateja na watanzania kwa ujumla pia watapata
fursa ya kushuhudia wanamuziki mastaa wa hapa nchini wakishirikiana na
wanamuziki wengine Afrika katika msimu wa pili wa kipindi cha Coke
Studio Afrika
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC1 na TBC2) kila siku za Jumamosi saa 3 usiku.
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC1 na TBC2) kila siku za Jumamosi saa 3 usiku.
Aliongeza kuwa promosheni hii inapatikana kwa wateja wa Vodacom Tanzania nchi nzima.
Post a Comment