Charlo Greene, ripota wa kituo cha runinga cha KTVA_TV cha huko
Alaska ameamua kutumia njia fupi ya ku-resign, baada ya kutangaza kuacha
kazi akiwa anaripoti ‘live’ kwenye runinga Jumapili usiku September
21.
“F— it, I quit,” ndio nena alilotumia hewani wakati anatangaza uamuzi wa kuacha kazi na kuondoka mbele ya camera.
Kwa mujibu wa the Alaska Dispatch News, Greene siku hiyo aliripoti
habari kuhusu ‘Alaska Cannabis Club’, club inayojihusisha na
kuwaunganisha watu wanaotumia marijuana kwa tiba, na baada ya kumaliza
kuripoti habari hiyo akajitangaza kuwa yeye ndiye mmiliki wa club hiyo
na kwamba anaacha kazi kwenye kituo hicho cha TV ili autumie muda wake
kupigania kuhalalisha marijuana huko Alaska.
Ghafla matangazo yalirudishwa kwa mtangazaji aliyekuwa studio
(anchor), ambaye alipatwa na mshituko uliomfanya ashindwe kuendelea
kuongea.
Kituo cha KTVA11 kiliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“Dear Viewers,
We sincerely apologize for the inappropriate language used by a KTVA
reporter during her live presentation on the air tonight. The employee
has been terminated.
Bert Rudman
News Director – KTVA 11 News”
Home
»
Entertaiment
» Video: Ripota aacha kazi akiwa anaripoti ‘live’ kwenye taarifa ya habari ya TV, ‘F**k it, I quit’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment