0
Ali Choki, Khalid Chokoraa, Super Nyemwela na wasanii wengine wa bendi wamewahi kujaribu kuimba kama solo artists lakini hawakuweza kufanikiwa lakini si kwa Christian Bella. Muimbaji huyo aliyeanza kujulikana na bendi yake ya Akudo, kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wanaopendwa zaidi nchini Tanzania.
IMG_0411
Mwaka huu, Bella amekuwa miongoni mwa wasanii waliopiga show za Kili Music Tour na Fiesta zilizokuwa zikiendelea katika wakati mmoja mikoa tofauti.
Jumamosi iliyopita alitumbuiza kwenye show ya mwisho ya Kili Music Tour iliyofanyika Leaders Club jijini Dar es Salaam na baada ya hapo alisafiri Jumapili hadi mjini Musoma ambako alitumbuiza kwenye Serengeti Fiesta mjini Musoma.
Sikiliza mahojiano tuliyofanya naye hapa.

Post a Comment

 
Top