0
Rapper Stamina amefunguka na kuelezea jinsi baba yake alivyomkatisha ndoto ya kucheza soka la kulipwa na kuamua kufanya muziki ambao hakuutegemea.
Stamina
Stamina ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaoperform kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta, Musoma Jumamosi hii, amesema alichaguliwa na wazungu pamoja na wenzake ili kwenda Afrika Kusini kucheza soka.
“Mpira ndio ulikuwa fani yangu kabla ya muziki,” Stamina ameiambia Bongo5. “Hata ukienda kuniulizia Morogoro nimechezea timu zote kubwa za Morogoro. Muziki nilikuwa napenda lakini ki siri siri sana, tatizo mipira ya Bongo mizengwe sana na pia mpira wa Bongo mpaka uje utoke utafanya kazi kubwa sana. Lakini kwa upande wangu kitu ambacho kilinifanya niachane na mpira, tulichezaga kombe moja la wazungu walikuja pale watu wa UN walikuwa wanataka watu watano, wanatafuta timu, ilikuwa ni Morogoro, Bagamoyo pamoja na Tanga wanatafuta kila sehemu watano watano ili wapatikane kumi na tano ili wapekekwe South,” amesimulia Stamina.
“Mimi nikawa nimechaguliwa kati ya watu kumi na tano, mzee ndo akaja kukatiza ndoto zangu. Baada ya kusikia nimechaguliwa na tayari ninaweza kwenda South mzee akanikataza kabisa, akasema ‘nataka usome’.Lakini alinisaidia kwa sababu aliniambia jambo la busara sana lakini kwa sababu tayari nilikuwa nimechaguliwa na mzee amenikataza, nikasema sitaki tena kucheza mpira kwasababu iliniuma sana ila sikuwa na jinsi kwa sababu kusoma ni muhimu sana kwa maisha ya sasa. Mpaka baadaye nilipoamua kufanya muziki na mpira nafanya kama mazoezi.

Post a Comment

 
Top