Pichani: Profesa Jay na Lil Ommy wa 100.5 Times Fm
Mashabiki wa Profesa Jay hivi karibuni wameshuhudia kionjo cha video
ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’ aliomshirikisha Diamond Platinumz na hivi
sasa wanaisubiri kwa hamu video nzima iliyoongozwa na Adam Juma wa
Visual Lab.
Rapper huyo mkongwe ameiambia Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm kuwa
tayari ameshakabidhiwa video hiyo na kwamba ni video kubwa na nzuri.
“Nimeshakabithiwa video ya Kipi Sijasikia na nimepata time ya
kuiangalia na Diamond Platinum. Ilibidi nimshirikishe muda wote kwa
sababu yeye ni mmoja kati ya waliofanya wimbo uwe wimbo… kusema kweli ni
bonge la video. Ile kiu ya watanzania na Afrika Mashariki kupata video
bora kabisa kwa kipindi hiki imewadia na kwa kweli kiu yao tunaikata.”
Amesema Profesa Jay.
Akizungumzia kuhusu mpango wa kuiachia rasmi, Profesa amesema kuwa
hivi sasa wanamalizia shows kadhaa katika ziara za Kili na baadae
watapanga uzinduzi rasmi utakaowahusisha watu mablimbali.
“Tunataka tuiache wikendi hii ipite lakini nadhani by next week
mashabiki wetu watajua lini tunaiachia na wapi itafanyika premier ya
wimbo huo kwa sababu tunataka tuwaite watu tofauti tofatu kwa sababu ule
ni wimbo wa watanzania. Sio wimbo wa Profesa Jay pekee…Kusema ukweli ni
video ambayo itakuja kuleta mapinduzi katika industry yetu na vitu kama
hivyo.”
Post a Comment