Muimbaji hiyo amedai kuwa ingawa hakuwa na pesa nyingi, anajivunia msaada alioutoa kwa baadhi wa wasanii na wakafika mbali.
“Unajua siku zote muziki ni kupanda na kushuka ila kikubwa zaidi ni kusaidia pindi unapomuona mwenzako anaomba msaada na wewe unahisi unaweza kumsaidia,” PNC ameiambia Bongo5. “Young Killer alinipigia simu akaniambia ‘broo nakuja Dar nataka nikutafute’, baada ya kuja akaniambia ‘broo mimi na hustle na muziki hivi na hivi, nifanyie mpango nirekodi studio yoyote’. Nikamwambia ‘poa mimi ninarekodi kwa Shebby’. Baada ya hapo mimi nikaongea na Shebby akafanya ngoma. Alifanya wimbo na Rich Mavoko ambayo nadhani ndo ulikuwa ni wimbo wake wa kwanza kwa producer wa hapa Dar. Ndio maana nikasema kuna leo na kesho kama unaweza kumsaidia mtu unaweza tu ukamsaidi bila kujali una kipato kiasi gani. Lakini ninachoshukuru Mungu bado Young Killer anaendelea kufanya vizuri.”
Post a Comment