0
Mwana FA ni moja kati ya wasanii wa Bongo Flava wachache sana walioamua kujihusisha na mchezo wa masumbwi aka boxing na kufanya mazoezi na wachezaji wa timu ya taifa ya ngumi.
Rapper huyo ameiambia The Chart ya 100.5 Times Fm kuwa ameanza kucheza boxing muda mrefu na kwamba inafaida nyingi kwake na ndio mchezo anaoupenda.

“Nafanya boxing muda mrefu na ni hobby. Mimi naishi maisha yangu unajua, kwa sababu Mwana FA nina shughuli zangu za kimaisha. Kwa hiyo boxing ni moja kati ya michezo ninayoipenda. Kiukweli unanisaidi kwa sababu inazidi kunitengeneza fitness ya mwili wangu, na pumzi zangu zinakuwa nzuri hata kwenda kuperform jukwaani nakuwa vizuri. Sina mpango wa kuprofessionalize boxing anyway.”

Post a Comment

 
Top