Latifa ambaye alishika nafasi ya pili kwenye shindano la Miss Tanzania 2013, pia alijumuika na mpenzi wake huyo katika kitengo cha MOI kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kutoa misaada kwa watoto wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Kupitia Instagram, Latifa ameandika kuwa Ben Pol ni mwanaume anayempa furaha.
“On this special day napenda kumshukuru Mungu,mama na baba kwa kukuleta duniani. Umekua ni mtu muhimu sio kwangu tu bali kwa familia,marafiki,na waTanzania kwa ujumla. Mwanaume mkarimu,mnyenyekevu,muelewa,mcheshi,mwenye upendo,moyo wa dhahabu,mtanashati,busara #Handsome_With_Brains ninayemfahamu,” ameandika Latifa.
“Thank you kuwa muongozo kwangu,wadogo zako na mtu yoyote..We ni mfano wa kuigwa, Mungu azidi kukubariki na akuongezee mengi Benard. Ntaandika mengi sana lakini yote hayawezi kuisha Mungu tu ndo anaeyajua niliyo nayo na alitukutanisha kwa sababu.. HAPPY BIRTHDAY rafiki yangu,muongozo wangu,msiri wangu, pacha wangu,mtu unipae furaha kila cku #Mzaziiii. Have a blast #firstborn @iambenpol #SUPER_MAN #HERO.”
Post a Comment